Jamaa wa miaka 72 atiwa mbaroni kwa kumnajisi msichana wa miaka 17- Homa Bay

Jamaa wawili katika kaunti ya Homa Bay wametiwa mbaroni kwa madai ya kumnajisi msichana wa miaka 17 Jumapili.

Mmoja kati ya jamaa hao wa miaka 72 anadaiwa kutekeleza unyama huo katika kijiji cha Kojwach, kaunti hiyo ya Homa Bay.

Mkuu wa polisi eneo la Rachuonyo  Mashariki  Jack Obuo amesema jamaa huyo aliyetekeleza uozo huo ameoa.

Katika kisa kingine kama hicho ni kuwa jamaa wa miaka 22 ametiwa mbaroni baada ya kupatikana akimnajisi mwanafunzi wa darasa la nane Alego .

Chifu Tom Ondieki amesema alipatikana akiwa ndani ya nyumba yake Kapeter .