Vimbwanga hivi! Amos Kimunya aondolewa kesi ya wizi wa milioni 60

EYcn6kYWAAMg0HI
EYcn6kYWAAMg0HI
Waziri wa zamani Amos Kimunya na watu wengine wawili wameachiliwa na mahakama baada ya miaka sita ya kushtakiwa kuhusiana na kesi ya ufisadi.

Mahakama ya ufisadi Nairobi ilitupilia mbali kesi hiyo iliyokuwa inawahusisha na unyakuzi wa mali ya umma yenye dhamani ya shilingi milioni 60.

Hakimu Felix Kombo katika umauzi huo amesema, walalamishi walikosa kuwasilisha ushahidi wa kutosha wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

“No prima facie case had been established against the accused persons and acquit all the persons charged in court,” amesema Kombo.

Kimunya ambaye ni mbunge wa Kipipiri alishtakiwa pamoja na Lilian Njenga, Jughae Waianaina .

Kimunya anadaiwa kuwa mwaka 2001 pamoja na Njenga waliitunuku kampuni ya Midland ekari 25 za shamba la Umma.

.