Bajeti ya kitaifa kusomwa na waziri wa Fedha Yattan Juni 11 mwaka huu

Taarifa kutoka kwa wizara ya fedha ni kuwa, bajeti ya mwaka huu 2020-2021 itasomwa na waziri wa Fedha Ukur Yattani mnamo Juni 11 mwaka huu.

Yattani atatoa mwongoza wa bajeti hiyo Alhamisi kulingana na taarifa ambayo imetumwa kwa vyombo vya habari kuanzia saa 3 jioni.

Taarifa hizi zinajiri wakati ambapo Yattani ameonya wananchi kutokana na kudorora zaidi kwa Uchumi wa taifa.

Huenda serikali ikalazimka kukopo zaidi pesa za kufanikisha bajeti hiyo mwaka wa kifedha.