Mtikisiko mkubwa wa uongozi wa kamati hizo unatarajiwa kufanywa kufikia siku ya jumanne . Kiranja wa upande wa walio wengi Irungu Kang’ata amesema wanakamilisha mabadiliko hayo na wanatumai kwamba yatakuwa tayari kufikia siku ya jumanne .
Miongoni mwa wale wanaolengwa ni maseneta saba waliopinga hoja ya kumuondoa Kindiki Kithure kam naibu wa spika wa senate .
Maseneta hao ni Kipchumba Murkomen (Elgeyo Marakwet), John Kinyua (Nyandarua), Samson Cherargei (Nandi), Susan Kihika (Nakuru), Aaron Cheruiyot (Kericho), Benjamin Langat (Bomet) na Kindiki mwenyewe .
Siku ya ijumaa maseneta wote wa Jubilee isipokuwa saba hao walipiga kura ya kumfurusha Kindiki kama naibu wa spika wa senate baada ya jumla ya maseneta 54 kuidhinisha hoja hiyo .
Kindiki alifurushwa kwa kutokuwa muaminifu kwa rais Uhuru Kenyatta ambaye ndiye kiongozi wa chama cha Jubilee .
Kang’ata hata hivyo amesema hapatakuwa na hila dhidi ya jamii yoyote katika kupendekeza mageuzi hayo katika senate lakini akaongeza kwamba baadhi ya waliopinga hoja hiyo watakiona cha mtema kuni.Cheruiyot yupo katika kamati ya PSC ,ambayo ni muhimu kwani huta maamuzi bungeni .pia ni mwanachama wa kamati za ICT, Kawi na Bajeti
Kinyua, Cherargei na Langat ni wenyeviti wa kamati za senate na huenda wakapoteza nafasi hizo .Kinyua ni mwenyekiti wa kamati ya ugatuzi na uhusiano kati ya serikali kuu na za kaunti na pia ni mwanachama wa kamati ya afya.
Charargei ni mwenyekiti wa kamati ya haki ,masuala ya kisheria na haki za binadamu ambayo wanachama wake ni pamoja na James Orengo na Okong’o Mogeni (Nyamira). Cherargei pia ni mwanachama wa kamati za ugatuzi na leba .
Langat ni mwenyekiti wa kamati ya elimu .seneta huyo wa Bomet pia ni mwanachama wa kamati ya shughuli za bunge na kamati ya kanuni na utaratibu . Pia yupo katika kamati ya Utalii na viwanda .