Simba kamili! Diamond awaposti Zari na Tanasha kwa kuunga mkono muziki wake

Msanii Diamond Platnumz sasa anaonekana yuko kwenye mawasiliano mema na 'baby mama'  wake Zari Hassan na Tanasha Donna. Kwenye mitandao ya kijamii, Diamond aliposti vieo ya Zari na mwanawe Tiffah wakiusakata wimbo wake wa Quarantine.

Awali msanii huyo aliwaposti wanawe wakiucheza wimbo huo huku akiwaacha wengi wakisema wameruadiana na Zari.

https://www.instagram.com/p/CA3g-8UDW4z/

Mnamo Juni 1, Tanasha alirekodi video ya msichana akiucheza pia wimbo huo na kisha kumtumia Diamond ambaye naye aliposti kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Baaada ya kuposti aliandika ujumbe mfupi.

"THANK YOU FOR THE CLIP TANASHA DONNA. QUARANTINE MOVES WORLDWIDE HIT."

Sasa ni wazi kuwa Tanasha hajampa Diamond block kwenye mitandao ya kijamii  baada ya kumpa block baada ya kutengana mapema mwaka huu.

Akiwa kwenye mahojiano Tanasha alifichua kuwa alimuacha Diamond kwa ajili ya udanganyifu.

"Ilipofika kiwango kile cha ukafiri niligundua kuwa napigana na hao watu peke yangu, nilimuuliza kisha nikampa block na nikamaliza uhusiano wetu

Ilikuwa mwisho wangu mimi kwa maana nilikuwa mwaminifu kwake kama mwendawazimu, ilikuwa bora kwangu kutoka kwenye uhusiano huo kwa ajili ya mwanangu na kwa ajili ya amani ya akili yangu." Alizungumza Tanasha.