Hofu ya serikali! Maeneo ya burudani yapuzilia mbali masharti yaliyowekwa

JqPbD3XUYXMo688R.jfif
JqPbD3XUYXMo688R.jfif
Serikali imeelezea hofu yake kutokana na baadhi ya wakenya ambao wamekuwa na hulka ya kufurika katika mikahawa mbalimbali nchini kujiburudisha licha ya taifa kuendelea kusajili idadi kubwa ya maambukizi.

Kulingana na katibu katika wizara ya afya Rashid Aman wakenya wanalichukulia agizo  la kutotangamana kwa makundi  kama jambo lililotupiliwa mbali na serikali.

“I am sure that you have seen some video clips on social media showing people crowding in such places throwing all caution to the wind. This is flirting with danger. It creates the perfect environment for infections. We must not allow ourselves to quickly recede to the old way of doing things ,” alisema Aman.

Kamati ya kukabiliana na majanga ya kitaifa National Emergency Committee NERC imefunga klabu ya burudani ya 1824CLub baada ya video kuibuka mitandaoni ikionyesha namna wakenya waliokuwa wanajiburudisha siku ya Madaraka licha ya kuwepo na hofu ya virusi vya corona nchini.

Aman alisema kuwa serikali imeruhusu tu maeneo ya mankuli yaani eateries na mikahawa mingine kuendelea na shughuli zake japo kwa kuzingatia masharti ya wizara ya afya.

Wizara ya usalama wa ndani kupitia ukurasa wake wa Twitter ilielezea ni kwa nini kumekuwepo na ongezeko la virusi hivyo katika mtaa wa Lang'ata baada ya kutweet video ya watu wakijivinjari bila kuzingatia maagizo ya serikali.

NationalERKe

 

@NationalERKe

  No one should be surprised why we have cases rising in Langata.Our young people have decided not to follow the Government guidelines. And obviously a greedy Kenyan who does not care whether people contract the disease or not.

 Aman pia alisikitikia baadhi ya wakenya ambao wamepuuzilia mbali wazo la kuvalia barakoa na wengine kukosa kuzivalia ipasavyo.

“They are like chin guards…we also notice people who wear the mask and only cover the mouth.This is unacceptable!”Alisema Aman