Tafakari! Mwanamume amnajisi mwanawe wa miaka 16 na kumgonga na kifaa butu kichwani

CRIME-SCENE
CRIME-SCENE
Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Mbooni Mashariki kaunti ya Makueni sasa wameanzisha msako mkali dhidi ya jamaa mmoja aliyemnajisi mwanawe wa miaka 16 na kisha kumgonga kwa kifaa butu kichwani baad ya kutekeleza unyama huo.

Chifu wa kata ya Kinze Kimeu Kituu amesema baada ya majirani wa jamaa huyo kusikia mvutano uliokuwa unatokea ndani ya nyumba yake, waliamua kwenda kutazama kilichokuwa kinajiri na kumpata mwathiriwa akiwa amepoteza fahamu huku damu ikimtoka kichwani.

Aidha nguo zake na kitanda ambacho jamaa huyo alikuwa amefanyia uovu huo zilikuwa zimejaa damu huku damu nyingine ikitoka katika sehemu nyeti za mwathiriwa.

“Other signs indicated she had been hit in the head with a blunt object, causing her instant fainting,” amesema Kituu.

Jaribio la jamaa huyu kujitia kitanzi limeambulia patubu baada ya maafisa wa polisi kumpata akiwa hai ndani ya nyumba yake na kupelekwa katika hospitali kuu ya Mbooni ambapo ilibainika kuwa alikuwa amekunywa sumu.

Katika nyumba hiyo vile vile maafisa hao wa polisi wamepata barua inayodaiwa kuandikwa na jamaa huyo ya kujitia kitanzi.

Katika barua hiyo aidha mshukiwa anasema yeye  na mwanawe walikuwa wameamua kujitoa uhai kutokana na hali ngumu ya maisha.