Visa 187,800 vya corona vimesajili katika bara Afrika- WHO

Maambukizi ya virusi vya corona yanaendelea kukita kambi katika mataifa ya Afrika huku shirika la Afya duniani likiripoti kuwa kufikia sasa waafrika 187,800 wameambukizwa virusi hivyo hatari.

WHO pia imesema kuwa watu 82,400 wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata nafu huku wengine 5,100 wakiwa wamefariki kufikia sasa kutokana na virusi hivyo.

Licha ya taifa la Afrika kusini kuongoza kwa idadi kubwa ya maambukizi ndilo taifa la kipekee lililosajili idadi kubwa ya watu waliopona kutokana na virusi .

Matifa mengine yaliyosajili visa vingini ni kama Misri na Nigeria.

Kufikia sasa Kenya imesajili visa 2767 vya maambukizi ya virusi hivyo.