Inaitwa co-parenting,' Zari Hassan awaambia Watanzania baada ya kusema anataka kurudiana na Diamond

jBCk9kpTURBXy9lNGQzYzNmNjQyMzlkNjljMmFkMGI3OTk2YzBiOWMxMy5wbmeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
jBCk9kpTURBXy9lNGQzYzNmNjQyMzlkNjljMmFkMGI3OTk2YzBiOWMxMy5wbmeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
Mwanabiashara na aliyekuwa mpenzi wa Diamond Zari Hassan ametupilia mbali madai kuwa wamerudiana au anataka kurudiana na Diamond baada ya kusuluhisha tofauti walizokuwa nazo.

Zari alisema, kwa sababu wanazungumza na baba wa watoto wake hawajarudiana pamoja, aliweka wazi kuwa wanasaidiana kuwalea watoto wao na wala si kurudiana na Diamond huku akisema watoto wake wanapaswa kupata upendo wa wazazi wote wawili.

Pia aliwasuta watu ambao wamo juu chini kuchunguza maisha yake na kumwambia jinsi anavyopaswa kuishi.

Mama huyo aligadhabishwa na watu ambao wanasema ana tamaa ya kurudiana na Diamond licha ya watoto wake kuwa na mawasiliano mema na baba yao.

"“Ooh she is so desperate to get back with him, No. Wacha niwafundishe kitu kimoja haswa watanzania nataka muingia kwenye tafsiri za google

Inaitwa co-parenting  kwa ajili ya watoto ambao mnao mkiwa wawili si mambo ya kuwa oooh ana tamaa ya kurudiana na yeye wala anapigana sana kurudiana na yeye

Na kumfanya kuonekana kuwa anataka kurudiana na mimi, kwa nini mna machungu ya kwamba mtu ameamua kuwasaidia watoto wake

Kwa nini mnaumia, hili jambo linakuja kutoka Tanzania mtu ana tamaa aje wanapoamua kuwalea watoto wao pamoja." Zari alieleza.

Alizidi na mazungumza yake kwenye mitandao ya kijamii ya Instaram,

"Diamond hapaswi kuthibitisha upeo wake kuwa anataka kurudiana na mimi, na mimi sipaswi kuthibitisha kuwa nataka kurudiana na Diamond

Ambacho tunafanya sasa ni kwa manufaa ya watoto wetu, watoto wangu wana furaha kwa sababu ya baba yao kuwapigia simu kila mara

Haswa Tiffah hufurahia sana huku akisema thats my papa calling, huwa anazungumza na wao, kuwachezea piano pia anafanya kila kitu awezalo, shida mbona nyinyi mnaumia."

Zari alisema kuwa Diamond aligundua makosa yake na anajaribu kurekebisha kivyovyote vile;

“And to set the record very straight am not back with Diamond, Diamond is not back with me, we are co-parenting. There are two kids involved, we both realized out mistakes and out priority right now is our kids. He gonna fetch tham , he gonna sent someone to take them or I’m gonna sent them with my bother to come to Tanzania, it’s how it’s supposed to be its called a parental plan, sio lazima kurudiana." Alisema.

https://www.youtube.com/watch?time_continue=175&v=F0lTwstYrTw&feature=emb_title