David Luiz: Defenda wa Arsenal asema kushindwa kwao mabao 3-0 na Mancity ni kwa sababu ya makosa yake

Mlinzi wa kilabu ya arsenal  David Luiz  amekubali kuwajibikia  kushindwa kwao mabao 3 kwa  nunge na Manchester City  lakini  akasema yungali ana matumaini ya kuichezea kilabu hiyo.

Luiz,  ambaye mkataba wake unatamatika mwishoni mwa mwezi huu  aliondolewa uwanjani ili kutamatisha kurejea kwake uwanjani kuliozongwa na makosa chungu  nzima .

"Ni makosa yangu, timu ilifanya vyema  hasa ikiwa na wachezaji 10  kocha pia yuko sawa na yote ni kwa ajili ya makosa yangu" amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.

"Nataka kusalia hapa. Kocha anafahamu hilo ma anataka nisalie  hapa."

Luiz alijiunga na Arsenal  kipindi kilichopita cha uhamisho  kutoka Chelsea  kwa pauni milioni 8  na alikuwa ameachwa katika benchi  dhidi ya City kwa ajili ya kutoeleweka kuhusu hali ya mkataba wake.

Aliingia uwanjani katika dakika ya 24  baada ya  kujeruhiwa kwa  Pablo Mari na alifanya masihara yaliompa bao la kwanza   Raheem Sterling.

Kisha baadaye alihusika na kumbwaga chini Riyad Mahrez na kusababisha penalty  na kuonyeshwa  nje ya uwanja. Kufurushwa kwake kutoka mechi hiyo kunamaanisha ameichezea arsenal mchuano wake wa mwisho endapo hatazidisha mkataba wake.