Niko tayari kuwa baby mama wa nne wa Diamond Amber Lulu asema yuko tayari kumzalia Diamond

Staa wa bongo Diamond Platnumz licha ya kuwa na baby mama watatu kuna wale wanamhitaji sana awe baba wa watoto wao na wanafanya chochote kile ili kuhakikisha wamempata.

Diamond anaweza kuwa na miaka 30, lakini amefanya mengi katika miaka yake kuliko vile wengi wamefanya, pia ni miongoni mwa wasanii bora afrika mashariki na kufahamika sana na mashabki wake.

“Nampenda Mondi (Diamond) kwa sababu ni fighter, hustler lakini pia mwangalie amekata body. Ukimwangalia, unachanganyikiwa

“Akisema ananiona nakubali na natulia kabisa. Sasa hivi najibrand nataka niwe kama Zari na Tanasha. Naenda gym nikae vizuri. Wajua sina mtoto kwa hiyo mimi nataka nizae na Mondi.

Naskia Zari anataka kurudi, akirudi tutapambana, tutakuwa wake wenza, tutalea watoto wote.” Alieleza Lulu.