Niliacha kazi ili kumtunza mwanangu,' Mama yake DJ Evolve asema

Kwa muda wa miezi sita familia ya Orinda haijakuwa kama vile ilikuwa awali, hii ni baada ya Felix Orinda almaarufu DJ Evolve kupgwa risasi mapema mwaka huu.

Muda huo wote amekuwa amelazwa hospitali akipokea matibabu, hivi majuzi alitoka hospitali lakini anazidi kupokea matibabu akiwa nyumbani.

Jambo ambalo mama yake hajafurahishwa nalo huku akiamini kuwa mwanawe amepooza kutoka kiunoni kuteremka na bado anataka matibabu zaidi.

Akiwa kwenye mahojiano na mwanahabri wa runinga ya NTV alizungumzia vile maisha yamekuwa baada ya kupigwa risasi.

" Nina mhemko mwingi sana kwa sababu ya siku hiyo ya tukio hilo, nilipopokea habari kuwa mwanangu amepata ajali katika maeneo yake ya kazi nilishtuka sana

Nilihisi kila kitu kimebadilika, nilimuomba Mungu  nikamwambia kuwa ila kitu kishaatendeka,na ninaomba atakuwa nami kwa kila kitu na atamlinda mwanangu." Mama Evolve Alizungumza.

Mama Evolve alisema kuwa aliwacha kazi yake wakati DJ huyo alipopigwa risasi ili kumtunza.

"Tangu siku ya tukio hiyo niliacha kazi yangu na nikaanza kumtunza mwanangu, tumekuwa tukitegema wasamaria wema,kwa mkate wetu wa kila siku."

Alisema uwa hajawahi muona mbunge huyo na hangependelea kuzungumzia jambo hilo.

"Kwa ajili ya uchungu ambao ninao katika moyo wangu sitaki kuzungumzia jambo hilo,huwa tu nazungumza na Mungu wangu, maisha ya mtoto wangu yameharibiwa

Ni namatumaini kuwa nitapata haki ya mtoto wangu hayo tu." Alizungumza.

Pia alifichua kuwa Babu Owino alilipa millioni saba za gharama ya hospitali alizokuwa ameamrishwa na mahakama kulipa.

"Babu Owino alilipa millioni saba alizokuwa ameambiwa na mahakama alipe, mimi sikusema mwananangu atoke hospitalini kama vile wanahabari wengi waliripoti mimi si daktari

Inaweza kuwa aje mtu anaripoti habari kama hizo."

Babu alikamatwa baada ya tukio hilo na kuachiliwa kwa dhamana ya millioni kumi.kwa kweli hawakukosea waliposema mama ni mtu wa maana katika maisha ya mwanawe.