Miili ya watoto 2 yapatikana ikiozea ndani ya gari katika kituo cha polisi cha Athi River

26514934-117b-4e2a-af08-eb2f230baeed
26514934-117b-4e2a-af08-eb2f230baeed
Uchunguzi umeanzwa kufanywa kufuatia kisa ambapo miili ya watoto wawili mvulana na msichana imepatikana hii leo ikiozea ndani ya gari katika kituo cha polisi cha Athi River.

Mkuu wa kituo hicho cha polisi Catherine Ringera amesema watoto hao waliripotiwa kupotea Juni 11.

Watoto wa miaka kati ya 4 waliripotiwa kutoweka katika boma lao la KMC walipokuwa wanacheza na wenzao.

Baada ya kisa hicho kuripotiwa katika kituo hicho cha polisi, maafisa hao walianza kufanya uchunguzi hadi hii leo ambapo miili yao imepatikana ndani ya kituo hicho.

Taarifa zinadai kuwa miili hiyo iligunduliwa baada ya jamaa mmoja kwenda kudai gari lake lililokuwa limezuiliwa ndani ya kituo hicho.