Babu Owino hana ubaya, Babake DJ Evolve asema

babu-owino-DJ-Evolve-John-Orinda
babu-owino-DJ-Evolve-John-Orinda
John Orinda, ambaye ni babake  DJ Evolve amepinga madai kuwa mbunge wa Embakasi East Babu Owino hajakuwa akisaidia mtoto wake baada ya kumpiga risasi.

Oringa amesema kuwa mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele kuisaidia familia hiyo na hata kuwasiliana nao kila mara baada ya tukio hilo kutokea.

“Vile aliingia kwa nyumba naona iko improvement na iko dawa analetewa, yule anayeleta hizo dawa ni Babu Owino. Nurses wako naye mchana na usiku na hao pia ni Babu Owino aliprovide. Naona kama Babu Owino si mtu mbaya sana ingawa hatujakutana naye tuongee lakini hajapotea,” Oringa.

Amesema dawa ambazo mwanawe anahitaji kwa sasa ni ghali mno na ni mbunge huyo tu ambaye anauwezo wa kununua dawa hizo.

Mzee huyo amesema hayo katika kikoa na wanahabari akifichua kuwa japo mwanawe ameondoka hospitalini,angali anahisi machungu na kukataa tamaa ya iwapo atarudi katika hali yake ya kawaida.

DPP Noordin Haji alidokeza kuwa tukio hilo limemfanya mwathiriwa kupoteza sauti na hivyo kuwa vigumu kwake kuandikisha taarifa