Pikipiki ya Hussein Walugembe ilinaswa na polisi katika wilaya ya masaka siku ya jumatatu na akatakiwa kulipa rushwa ya takriban shilingi elfu 4 ili arejeshewe lakini hilo halikumfurahisha .idara nzima ya trafiki katika eneo hilo sasa ipo chini ya uchunguzi kwa mujibu wa msemaji mmoja wa polisi .
Pia inaripotiwa kwamba Walugembe alikuwa akiishi katika makaazi ya polisi na alikuwa akiwazuia maafisa hao chakula . Nchini Uganda usafiri wa boda boda umepigwa marufuku katika baadhi ya nyakati ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona na mara kwa mara polisi hufanya msako wa kuwakamata wahudumu wanaokaidi marufuku hiyo .
Wahudumu hao wanaruhusiwa kufanya kazi zao kuanzia saa kumi na mbili alfajiri na hadi saa kumi na moja jioni na wanaweza tu kusafirisha mizigo .
Polisi wanasema Walugembe alikuwa amempa rafiki yake pikipiki yake aliyepatikana akimsafirisha abiria hatua iliyosababisha kunaswa kwa pikipiki hiyo . Baadaye alifadhaishwa na kutibuka kwa juhudi zake kutaka pikipiki yake iachiliwe ndiposa akaamua kujifungia katika chumba kimoja ndani ya kituo cha polisi na kujiteketeza kutumia mafuta petrol aliokuwa ameficha kweye chupa .