Mama awauwa wanawe kisha kujiua baada ya kugombana na mumewe

mqsk9kpTURBXy9mZTkyZjVhZDJmY2NlNzFiZGRiZGM3YjQ5YmQ5ZDgxZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
mqsk9kpTURBXy9mZTkyZjVhZDJmY2NlNzFiZGRiZGM3YjQ5YmQ5ZDgxZC5qcGeSlQLNAxQAwsOVAgDNAvjCw4GhMAE
Ni tukio ambalo liliwaacha wakazi wa Kakamega wakiwa wameshika tama baada ya mama mmoja kujiua na kisha kuuwa wanawe baada ya ugomvi kati yake na mumewe.

Nduru za habari zanaarifu kuwa mwendazake alijitupa kwenye mto Nzoia na wanawe watatu kaunti ya Kakamega, mtoto moja anaendelea kupokea matibabu baada ya kunusurika kifo hicho.

Haya yanajiri wiki moja baada ya mama mmoja kutoka mtaa wa Naivasha kuwauwa wanawe wanne na kuandika habari jinsi alitekeleza kitendo hicho.

Kupitia kwa barua alikiri kuwa alikuwa amepagawa na mapepo ndiposa akafanya kitendo hicho, Beatrice Mwende Kimothoi alisema kuwa hafahamu nini kilimwingia ili aweze kuwauwa wanawe huku akisema kuwa  ni mapepo ambayo yalimshauri atekeleze kitendo hicho.

“We ate supper together and even watched TV before the children, whom I loved so much, went to bed only for the evil spirits to take over."

Kulingana na Mwende kila taerehe 26 ya kila mwezi angepagawa na mapepo ambayo hangeweza kuyathibiti, mnamo tarehe 6 Julai ripoti za daktari zilionyesha kuwa Mwende alipokuwa anatekeleza kitendo hicho alikuwa na shida za kiakili.

Je ina maana kuwa wazazi wamechoshwa na wana wao baada ya kuwa nyumbani kwa miezi nne?