Shughuli za PSC zapunguzwa baada ya 10 kupatikana na Covid-19

Tume ya utumishi  wa umma imepunguza shughuli zake ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona baada ya wafanyikazi wake 10 kupatikana na ugonjwa huo.

Kaimu mkurugenzi wa afya Patrick Amoth Jumanne alisema  hatua nyingine kama vile kuhakikisha kwamba wafanyikazi hao hawakaribiani wanapokuwa kazini zimechukuliwa.

“Tutaweka mikakati katika afisi  za serikali ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu’ amesema Dr Amoth .

Afisa mkuu mtendaji wa PSC Simon Rotich  amesema vipimo vilivyowalenga wafanyikazi wake vilionyesha kwamba kumi walikuwa na virusi hivyo.

Tume hiyo imesema oparesheni zake zitapunguzwa kwa siku 14 kuanzia Jumanne  na kuja afisini sasa kutadhibitiwa miongoni mwa wafanyikazi wa tume hiyo.