Baba Lao: Diamond Platinumz atikisa maungo na Hamisa na Wema katika usiku mmoja

Siku ya jumamosi  msanii Diamond Platinumz  aliandaa bash kubwa kwa hisani ya msanii wake wa kike Zuchu katia usiku uliowaleta pamoja wasanii wote tajika nchini Tanzania katika  paa moja .

https://www.instagram.com/p/CC0ASHAA651/

Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na  Lady Jay Dee, Mbosso, Juma Jux,  maneja wa Diamond  Sallam, Esma, Sandra Kassim, Rayvanny, Irene Uwoya, Jokate Mwegelo,  wapenzi wa Diamond  Wema Sepetu, Hamisa Mobetto miongoni mwa wengine wengi

Lakini kilichowapata wengi kighafla ni wakati Diamond alipoingia steji kupiga densi na Hamisa Mobetto  na baadaye akizungumza baada ya hafla hiyo alimlimbikzia Hamisa sifa nyingi sana ;

NASHUKURU MOBETTO STYLES NDIO WAMENIVALISHA.NI DESIGNER NA MIMI KAMA MTANZANIA NINA KILA HAKI YA KUSUPPORT WATANZINIA WENZANGU.

Wakati mmoja pia Diamond alipata fursa kwenye steji kuzinengua na mpenzi wake wa zamani Wema  walipokuwa wakiucheza wimbo a Mbossi ,Hodari .

https://www.instagram.com/p/CCzUP98gF1Y/

Video hizo  mbili sasa zinasambazwa mitandaoni na wengi wanangoja kwa hamu kuona wapenzi wengine wa zamani wa  Diamond Zari Hassan na Tanasha Donna watasema nini kuhusu video hizo