Kocha wa United Ole Gunnar Solskjaer alimuacha mkekani mlinda lango wake wa mechi za FA Sergio Romero ili kumpa De Gea kazi hiyo lakini masihara yake mawili yaliwafanya kushindwa kwani aliizawadi Chelsea mabao mawili
De Gea alifanya mchezo kujaribu kuokoa mkwaju wa Olivier Giroud katika kipindi cha kwanza kisha tena akatapatapa na mkwaju wa yadi 20 wa Mason Mount muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza .
Mchezo mzuri wa Chelsea ulipigwa jeki wakati nahodha Harry Maguire alipojipata amewavua mkwaju wa Marcos Alonso katika lango lake zikiwa zimesalia dakika 16 mchuano kutamatika .
Kikosi cha Frank Lampard Kilikuwa na uthibiti kamili kuanzia mwanzo wa mechi hiyo na walifaulu kumaliza msururu wa man unitedwa kutoshindwa katika mechi 19 kwenye mashindano yote .
Bruno Fernandes aliifungua the reds bao moja kupitia penalti lakini halikufuta chochote kwa sababu wino ulikuwa umeshakauka .