Baadaye aliwalaumu watu aliosema walimuonea wivu kwa kupewa kazi ya kuwafantia kampeini wanasiasa fulani .
Akizungumza na Maina kageni katika kipindi chake cha asubuhi ,Mr Nice amesema tukio hilo lilimshtua sana na hakulizungumzia kwa muda mrefu ili kuhakikisha kwamba kwanza yuko salama .
Alisema waliotaka kumuua waliomuonea wivu kwa sababu ya mafanikio yake .
Alisema hivi kupitia mitandao ya kijamii
‘ kampeini za kisiasa i jambo la kupita na maisha huendelea baada ya uchaguzi ,ni jambo baya kwamba mrengo wangu wa kisiasa ulinifikisha hospitalini
Akizungumza kuhusu hai yake ya kisasa ya kifedha Mr Nice alisema
“ tangu agostri mwaka jana nimekuwa napiga tours za muziki tanzania . pia nimeenda sudan kusini ,rwanda na burundi kabla ya janga la corona kuwa tatizo na kunifanya nifutilie mbali ziara hizo .
Mr Nice pia amejitetea kisema kwamba hatua yake ya kudidimia kimuziki haina uhusiano na uraibu wake wa kunywa pombe .
“ sijawahi kuwa na tatizo la kunywa pombe kupindukia ingawaje mimi hunywa ,hilo halijawahi kuvuruga taaluma yangu katika muziki
Akijibu madai kwamba hana nidhamu Mr Nice amesema
“ aliyetoa madai hayo lazima alinifanyia jambo ili kunifanya niwe hivyo