Kifaa hicho - dapivirine vaginal ring, ambacho bado kinatengeezwa kitawawezesha wanawake kuzuia kujitia katika hatari ya maambukzi katika hali ambapo wanakosa kutumia dawa za prophylaxis au PrEP.
PrEP ni matumizi ya dawa za antiretrovirals na watu wasio na HIV ili kuwazuia kupata maambukizi ya virusi hivyo .
Shirika la International Partnership For Microbicides limesema kifaa hicho kikitiwa katika sehemu ya uke ya mwanamke kitakuwa kikitoa pole pole dawa ya antiretroviral ya dapivirine kwa siku 28 .
Kifaa hicho kimetengezwa na silicon matrix polymer na kina dawa ya ARV dapivirine ambayo itakuwa ikitolewa pole pole kwa kipindi cha mwezi mmoja . Kifaa hicho kitatumiwa na wanawake walio na umri wa zaidi ya miaka 18 .
“ watalazimika kuweka kifaa kipya kila baada ya siku 28 pindi tu cha kale kinapoondolewa’ IPM imesema .
Dapivirine hupunguza hatarai ya maambukizi ya HIV-1 baada ya saa 24 za kuwekewa kifaa hicho .