Raila awataka maseneta kuunga mkono mfumo wa CRA wa ugavi wa mapato

uHURU RAILA
uHURU RAILA
Kiongozi wa ODM  Raila Odinga amewataka maseneta kupitisha  mfumo wa ugavi wa mapato ulipendekezwa na tume ya CRA

Kupitia taarifa  Raila   amesema senate inafaa kuruhusu taifa kundelea  mbele baada ya kushindwa kupata mwafaka kuhusu mbinu inayofaa kutumiwa kugawa pesa hizo kwa kaunti . marekebisho ya mfumo huo yalikuwa yamependekezwa na  senate.

" Chini ya hali hii nchi yetu na wananchi  sasa watahudumiwa vyema endapo  tutatumia mfumo uliokuwa umependekezwa na  tume ya CRA’  amesema Raila

Raila  amesema masuala mengine yanayoibuliwa yanaweza kupelekwa kwa CRA Ili kuzingatiwa katika siku zijazo .

Taarifa ya Odinga imejiri baada ya kuzuka mgawnayiko kati ya  maseneta kuhusu jinsi pesa za kauti zinazofaa kugawanya baada ya kuzuka tofauti kuhusu mbinu mbili za kutumika katika kuamua kiasi ambacho kila kaunti itapokea .

Kiraranja wa wengi katka senate Irungu kangata hata amenukuliwa akisema kwamba akisema mwafaka wa handshake utakuwa hatarini endapo mfumo unaopendekezwa na serikali hautapitishwa .