Maureen Waititu azungumza kuhusu kujitosa tena katika mapenzi baada ya kutengana na Frankie

maureen-waititu-and-frankie-696x418
maureen-waititu-and-frankie-696x418
Maureen Waititu  sasa amesema amemuachia mola  kuamua hatima yake kuhusiana na masuala ya kujitosa tena katika mapenzi  baada ya miezi kadhaa tangu kutengana na  baby daddy  wake Frankie .

Akizungumza na MC jessy ,mama huyo wa watoto wawili  amesema endapo Mungu atampa mwanamme mzuri  ,basi hatokuwa na buidi ila kukubali na kuendelea na maisha .

 “ SO  NI JAMBO RAHISI SANA ,HII SIO SAFARI YANGU TENA NA NAMUAMINIA MUNGU  ANIPELEKE ATANAKOTAKA . KAZI YANGU ITAKUWA KUMUAMINI NA KUMFUATA .

 IWAPO ANA  MPANGO NA MIMI KWAMBA NITAKUTANA NA MTU  AMBAYE …. NA NIAMINI KAMA BINADAMU NINA MATAMANIO  NA NAJUA NACHOTAKA SIKU ZIJAZO  ,LABDA HATA SIJUI KWA SABABU FIKRA ZANGI ZINABADILIKA .

 ANAKONIPELEKA NI SAWA .IWAPO NITAKUWA NA MTU AU LA ,NATAKA TU KUWA NA FURAHA  NA NIWE MAMA MZURI

Frankie  na  Maureen  walitengana kwa sababu ambazo  wao wanazijua  na tayari Frankie keshajitosa katika uhusiano mwingine.

Anataraji kupata mtoto wake wa tatu na  mwanasosholaiti mwingine wa Kenya  Corazon Kwamboka.