Kamanda wa polisi aliyemshutumu Sonko kwa kumshambulia aletwa Nairobi kuwa mkuu wa Polisi

Ndolo
Ndolo
Rashid Yakub amehamishwa hadi  Nairobu kuwa mkuu wa polisi kutoka kwa Philip Ndolo.

Mabadiliko hayo yameangazwa siku ya jumamosi  na Ndolo ataelekea Nyeri kuwa naibu kamanda wa chuo cha mafunzo ya polisi Kiganjo .

Yakub alikuwa kamanda wa polisi wa pwani na  disemba mwaka jana alimshtumu gavana wa Nairobi Mike Sonko kwa kumshambulia wakati Sonko alipokuwa akikamatwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Voi  kuhusiana na kesi ya utoaji  zabuni  ya shilingi  Milioni 357 .

Baadaye Yakub aliamua kuondoa kesi hiyo dhidi ya Sonko