Kutoka Papa Dennis hadi kwa Njenga Mswahili tazama Celebs wote walioaga dunia wakiwa maskini

Kifo cha msanii wa gospel Papa Dennis  kimefichua jinsi wasanii wengi wanavyoteseka katika lindi la umaskini licha ya wengi  kufikiri kwamba wana pesa kwa ajili ya mtindo wa  maisha yao .

Hii hapa orodha ya baadhi ya wasanii na celebs taika ambao vifo vyao vilifichua jinsi hali ilikuwa ngumu kwao

  1. Papa Dennis

Kifo cha Papa  Dennis kiliwashtua wengi baada ya mwili wake kupatikana huko Pangani . Papa alionekana kuwa a yote ikizingatiwa kwamba alitokea Gheto na kufaulu kujipata katika ulingo wa  muziki .

Baadaye alifukuzwa kutoka nyumba yake aliokuwaamepangisha  bada ya kukosa kulipa kodi na kisha kuanza kuihi kama skwota pangani katika studio za kurekodi muzik kabla ya kifo chake .

  1. Mzee Ojwang

Kwa watoto waliozaliwa miaka ya 80 na 90 hakuna asiyemjua mzee ojwang’ na jinsi alivyokuwa  akiwapasua mbavu kwa vituko vvyake katika kipindi cha Vioja mahakamani .

Kwa muda mrefu alikuwa akiigiza pamoja na mama kayai  . Aliaga dunia julai mwaka wa 2015  baada ya kupata maradhi ya numonia . kabla ya hapo alikuwa ametibiwa baada ya kuanza kupata matatizo ya macho na serikali ikaifutilia mbali bili ya matibabu yake katika hospitali ya KNH

  1. Achieng Abura 

Achieng aliaga dunia oktoba mwaka wa 2016 katika hospitali ya KNH .kabla ya kifo chake  alikuwa ameitisha hafla mbili za michango  na watu wengi walijitokeza kutoa pesa za kumsaidia kupokea matibabu yake .

Katika mahojiano alimueleza Biko Zulu kwamba alikuwa akipata matatizo ya kupata pesa za kumpeleka mtoto wake  kwa matibabu nchini Uingereza  mwanae alikuwa na anemia.

Na katika hafla moja ya kuchangisha pesa chini ya watu 10 ndio waliojitokeza  nan i baada ya kifo chake ndipo kila mtualitaka kutajwa pamoja na jina lake kubwa .

  1. Joe Kadenge

Mwanasoka stadi sana Joe Kadenge  aliaga dunia katika hospitali ya Merdian ,Nairobi

Kulingana na mwanawe Oscar ,afya ya bbake haikuwa nzuri kwa muda mrefu  na kwa mtu wa taadhima na sifa zake  wengi walishangaa jinsi alivyotelekezwa  kwani akitbiwa NHIF ililazimika kumlipia bili ya shilingi milioni 2

Kinaya ni kwamba licha ya kuhitajimsaada akiwa hai ,bajeti yake ya mazishi iligonga shilingi milioni 5.

  1. Njenga Mswahili

Mchekeshaji huyo wa Churchill aliaga dunia Novemba mwaka wa 2019  baada ya kugongwa na treni .

Wengi walijua kama  Njenga Mswahili – jina halisi James Anthony Njenga –  na mwili wake uliobabadiwa ulipatikana katika mkondo wa treni mtaani Dagoretti .

Njenga  alifahamika kwa kutoa ucheshi wake katika lugha ya Kiswahili ndiposa alipewa jina hilo –mswahili .kabla ya kifo chake  alikuwa amepatwa na msongo wa mawazo  na kwa bahati mbaya hakitajulikana kilichomtia katika hali hiyo .