Tangazo hilo linajiri siku chache tu baada ya bunge la taifa kupunguza shughuli zake kwa hofu ya wafanyikazi na wbaunge kuambukizwa ugonjwa huo. Spika wa senate Ken Lusaka amesema mikutano yote inayowalazimu maseneta kukutana ana kwa ana imefutiliwa mbal kwa mwezi mmoja ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo .
Spika amesema hali itatathminiwa baada ya mwezi mmoja na kamati ya senate kuhusu uhasibu ndio inayoweza kuandaa mikutano kila baada ya muda Fulani inapohitajika .
Wiki jana spika wa bunge la taifa Justin Muturi alipiga marufuku mikutano yote ya kamati na kushauri dhidi ya mikutano yote ya ana kwa ana katika majengo ya bunge . Agizo hilo lilitolewa baada ya kuibuka ripoti kwamba huenda wabunge kadhaa na wafanyikazi wa bunge wameambukizwa ugonjwa wa corona .
Jumanne iliyopita kiongozi wa wachache bungeni John Mbadi alifichua kwamba wafanyikazi 36 wa bunge wamepatikana na Covid 19