Tisa wafariki nchini India baada ya kunywa sanitiser

Watu tisa wameaga  dunia nchini India baada ya kunywa sanitizer ya kutakasa mikono  baada ya duka za kuuza pombe katika mji wao kufungwa  kama mojawapo ya kuwazuia watu kulewa wakati nchi hiyo inapokabiliana na janga la corona .

Watiu hao walipoteza fahamu baada ya kunywa sanitizer  iliyochanganywa na soda  na  maji  amesema mkuu wa polisi wa  Siddharth Kaushal   wa mji wa  Kurichedu   katika jimbo la   Andhra Pradesh.

Walikimbizwa hospitalini lakini wakatangazwa kuaga dunia pindi tu walipofikishwa  .

Kundi hilo lilimua kutumia saniser kama kileo baada ya maeeo yote ya kuuza pombe kufungwa kufuatia agizo la serikali ya watu kutotoka nje ili kukabiliana na janga la corona .

Mamia ya watu huaga dunia kila mwaka nchini india kwa kunywa pombe hatari yenye sumu ambayo huuzwa kwa bei ya chini .

Wagemaji wakati mwingi huweka  methanol kupindukia katika pombe  na hata mafuta jambo ambalo husabaisha vifo vya watu wanaoitumia pombe kama hiyo ili kuzidisha kileo ndani yake .