Wanawake,4,hawanitoshi-Msanii Mbosso anong'ona

Msanii wa bongo Mbosso hayuko tayari kuoa mwanamke mmoja au wanne kama vile wamekubaliwa na dini ya waislamu, Mbosso alisema kuwa ana uwezo wa kuoa wanawake ishirini.

Alisema haya alipokuwa amehudhuria harusi ya dada yake staa wa bongo Diamond Platnumz.

"Bachela kama sisi tukiona hafla na harusi kamaa hii inatupa hamu ya kuoa, nafikiri kuwa nitapata wanawake wazuri hapa huwezi jua kama pia nitapata mke hapa

Kwa kuwa mwaminifu sifikiri kuwa wanawake wanne watanitosha wala kunitosheleza nikieza pata 20, au kumi au kuni na watano ni sawa lakini wanne hawatoshi." Alizungumza Mboso.

Msanii huyo tayari ana watoto watatu kutoka kwa wanawake tofauti, dada yake Diamond alifunga pingu za maisha kama mke wa tatu.