Safari yake ya kupona na kupata haki imekuwa ndefu na yenye machungu kwa sababu kando na pesa nyingi anazotumia kuwa matibabu yake ,mshukiwa alikwepa na kwenda Sudan Kusini alipomfanyia unyama huo .
Teresa anasema ulimwengu ulimpindfuka na kumuacha hoi miaka miwili iliyopita wakati mazungumzo yasio na hila kati yake na mwanamme huyo ili kukatiza uhusiano wao yalipotumbukia kuwa janga kwake .Anasema wakati walipoanza uhusiano hakujua kwamba jamaa huyo kwa jina Japheth alikuwa na mke . Baadaye alipofahamu ukweli kwamba Japheth alikuwa na mke ,Teresa alimtaka wakatize uhusiano wao lakini kumbe Japheth hakulichkulia kwa wepesi suala hilo na baadaye akapanga jinsi ya kumuadhibu Teresa akimlaumu kwa kuhitimisha uhusiano wao.
Japheth siku chache baadaye alimvizia Teresa akiwa nyumbani kwake na kummininia acid kwenye sehemu zake siri baada ya kumzidi nguvu na kumtoa nguo . pindi baada ya ukatili huo wake alitoroka na baadaye ikaripotiwa kwamba alikimbilia nchi jirani ya Sudan Kusini alikokuwa akifanya kazi . Baada ya tukio hilo Teresa alianza safari ndefu ya kuanza matibabu kwani acid hiyo ilimdhuru ngozi katika uke wake na kumfanya kuhitaji upasuaji maalum .
Anasema uchungu aliyopitia akipokea matibabu tangu sasa humfanya wakati mwingine kutaka kujiua lakini jamaa zake na rafiki zake wa karibu ndio wamekuwa wakimpa himizo la kuendelea kutaka kuishi . Aliwekea vifaa maalum vya kwnda haja ndogo na dawa ambazo yeye hupewa kila mara kutuliza maumivu zinamfanya kupata matatizo mengine kama vile kupoteza fahamu . Anasema katu hajawahi kusikiza mwanamume aliyechukulia kwa hasira habari za kuchwa na mpenzi wake na kuamua kuchukua hatua kama hiyo na tangia tukio hilo Teresa ameapa kwamba hatowahi tena kupenda .