Tenda wema nenda zako:Diamond amnunulia shabiki wake pikipiki baada ya kumpigia magoti

Shabiki mkubwa wa msanii wa Bongo, Diamond Platinumz ambaye alimpigia magoti na kumuomba amnunulie pikipiki, sasa ni mwingi wa tabasamu baada ya msanii huyo kutimiza haja ya moyo wake.

Jamaa huyo ambaye ni mchuuzi wa sambusa, bagia na vyakula vingine, alimkimbilia Diamond siku ya Jumanne, Agosti 11, wakati alipohudhuria hafla ya kuzinduliwa kwa Safe Travels.

Anamshukuru kwa kazi yake njema kabla ya kupiga magoti na kuomba msaada wa pikipiki ili amsaidie baba yake lakini Diamond anaonekana kumnyanyua na kumuagiza mmoja wa wasaidizi wake kumpa pesa kutoka kwenye gari.

Ni hafla ambayo ilikuwa imeandaliwa na bodi la utalii nchini humo ambapo iliudhuriwa na wanamuziki kadhaa ikiwemo Harmonize.

Baada ya kupewa pesa hizo shabiki huyo alimuombea Diamond baraka tele katika maisha yao.