Nilimpeleka Rich Mavoko kwa mganga afanikiwe maishani-aliyekuwa meneja wake afichua

rich mavoko
rich mavoko
Huku akiwa kwenye mahojiano na EATV, aliyekuwa meneja wa staa wa bongo Rich Maviko, Maneno alifichua mambo ambayo wengi hawakufahamu huku moja wapo ikiwa alimpeleka staa huyo kwa mganga ili afanikiwe maishani.

Maneno pia alidokezea kwamba walitofautiana na msanii huyo kisha wakanyamaziana kwa muda wa miaka sita bila ya kusemezana licha ya kukutana ana kwa ana katika shughuli za usanii.

Aidha alibainisha kuwa sasa msanii huo hatumii nguvu za uchawi na hayo ni ya zamani,

"Kwa Mganga tulienda kwa sababu zile zilikuwa mbinu za njia za kupita ili kuweza kufanikiwa, usitegemee kutuona tena kwa waganga ila tegemeeni kuona muunganiko mzuri kwetu na kumuona Rich Mavoko anakwenda sehemu nzuri, mambo mengine yote yamepita na tumeweza kusuluhisha." Alidai Maneno.

Maneno pia alimshauri Mavoko kuendelea kuachilia ngoma baada ya nyingine kwani yeye ndiye mfalme wa mziki Tanzania na mashabiki wake wanamuhitaji.

Pia alimtaka Mavoko awe mwenye heshima kwa wakubwa wake ambao wamewekeza pesa zao kwenye usanii wake.

Mavoko alitangaza kurejea kwake kwenye ulingo wa mziki kwa vishindo mnamo mapema Agosti 2020, huku akiwachia kuachia ngoma ya Babilon baada ya kusalia kimya kwa miezi kumi.

Mavoko alitoka katika lebo ya WCB na kukimya kwa muda huku mashbiki wake wakishindwa haswa nini kilitokea, bali alisema kmya chake alikuwa anaandaa vibao ambavo sasa yuko tayari kuvitoa.