Pigo kubwa kwa Mungatana baada ya uamuzi mpya wa korti

Mungatana
Mungatana
Aliyekuwa Mbunge wa Garsen Danson Mungatana na mwanabiashara mwenzake Collins Waweru wameshtakiwa kwa udanganyifu, wakili wa wawili hao alisihi mahakama kuacha mashtaka hayo na kisha kuzungumza na mlalamikaji nje ya mahakama.

Hata hivyo mashtaka yalikataa huku yakisema kuwa makosa ya wawili hao yalikuwa ya jinai.

"Wizara ya ulinzi inahusika kama mlalamikaji, kwa vile wanataka kupatanisha na mlalamikaji mashtaka mengi ni ya serikali."

Jumatano Mungatana alishtaki kwa udanganyifu katika mahakama ya Kibra baada ya ombi lake kutupiliwa mbali la kusikizana na mlalamikaji nje ya korti.

Kulingana na jaji Abdul Lorot ombi lake lilikosa ustahimilifu hivyo basi alibidi kutupilia mbali.

"Walikuwa na makubaliano yao lakini wameshtakiwa kwa maana mashtaka yameafikiana na kizingiti cha maslahi ya umma." Alisema.

Mungatana na mwenzake waliachiliwa kwa dhamana ya shillingi 200,000 baada ya kukana mashataka hayo, huku wakishtakiwa kwa udanganyifu wa hati na hata kupokea pesa kwa kujifanya.