'Tuliachana na Jacque Maribe nikiwa jela,'Jowie azungumzia uhusiano wake na Maribe

Msanii Jowie Irungu amefichua na kusema kuwa waliachana na mwanahabari Jacque Maribe alipokuwa jela hii ni baada ya kukamatwa kama mshukiwa mkuu wa mauaji ya mwanabiashara Monica Kimani.

Akiwa kwenye mahojiano Jowie alisema kuwa aliamua kuto zungumza na Jacque ambaye wakati huo alikuwa mpenzi wae baada ya kutengana.

Alisema kwamaba walikuwa wanaongea mara moja alipokuwa anamjulia hali yake.

"Huwa si zungumzii na Jacque kwa maana tulitengana nilipokuwa jela, kwangu hamna kitu kilichokuwa kinaendelea bali nilikuwa na Mungu wangu

Huwa hatuzungumzi labda mara moja kumjulia au kujuliana hali chochote ambacho mtu anatenda na kufanya haijalishi kuwa wewe ni mwanahabari, mtangazaji au msanii bora umemuingiza Mungu

 

Na Mungu ndiye amenitoa na ndiye atanitoa hayo ndio naamini." Alizungumza Jowie.

Haya yanajiri takribani miezi sita baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya millioni mbili, baada ya kufungwa jela kwa mwaka mmoja na nusu.

Wengi walimfahamu Jowie alipokuwa anamchumbia mwanahabari Jacque ambaye wakati huo alikuwa anfanya kazi na ringa ya Citizen Juni 2018, kisha wakamfahamu zaidi baada ya kuhusuka katika mauaji ya Monica KImani.