Ilikuaje: Sina marafiki nilidhani nina marafiki-Jowie Irungu azungumza

Katika bustani ya Massawe hii leo tulikuwa naye Jowie Irungu ambaye ametoa kibao chake na kupokelewa vyema na wakenya hii ni baada kutoka jela.
"Niliimba kibao hicho kwa maana nilikuwa nashukuru Mungu si kwa ajili ya mambo ambayo nilipitia awali bali nilitoa ili kibao hicho kiweze kunishilia

Si yuko katika tasnia ya nyimbo za injili kabisa."

Pia alisema kuwa hana kinyongo na mtu yeyote kwa yale yote amepitia na Mungu ndiye anajuwa sababu ya jambo kutendeka katika maisha ya kila mwanadamu.

"Usanii ni kitu ambacho nimekuwa nacho katika maisha yangu tangu kitambo, kwa sasa sina marafiki lakini nilifikiri nina marafiki si wote ambao walikuja kunitembelea nilipokuwa jela, lakini namshukuru Mungu kwa maana aliniwezesha."

Pia alisema kuwa hataki kupendwa na kila mtu wala kudharauliwa na kila mtu.

"Mimi napenda Mungu sana, ata nikiwa kamiti nilikuwa naomba sana, baada ya kutoka Kamiti sikuenda kwa daktari ili kupata ushauri wowote."Jowie Irungu Aliongea.

Jowie alipoulizwa kama anajutia maisha yake ya awali alisema hapama

"Do you regret your past." Massawe Alimuuliza.

"Hapana sijutii maisha yangu ya awali, kwa sasa niko na amani na natafuta kuwa na furaha, alisema Jowie.

Alisema wakati wake Mwingi anataka kutumia kumtumikia Mungu na kuwa karibu naye.akizungumzia uhusiano wake na Jacque Jowie alisema kuwa hawazungumzi sana kwa maana anatumia simu ya mkewe.

"Nafikiri laini ya simu yangu ina watu kumi na watano, neema ya Mungu huwa inajitokeza mara mbili, sina kinyongo na Jacque."

Jowie aliwashauri watu na mashabiki wazidi kuomba.