Sikujua kama Jowie angeimba,Jacque sitishio kwangu-mkewe Jowie Eleanor Musangi asema

117915346_191990185604423_987166888133165319_n
117915346_191990185604423_987166888133165319_n
Akiwa katika mahojiano na radiojambo mkewe Joseph Irungu almaarufu Jowie,Eleanor Musangi alisema kuwa hakujua kuwa msanii huyo angeweza kuimba na kuwa wamekuwa naye kwa muda mrefu.
"Wimbo wa nishikilie Jowie alijiandikia mwenyewe tumekuwa naye kwa muda mrefu, vile watu huona Jowie si yule najua kwa maana ni mcheshi mwema

Pia mimi meneja wake huwa najiuzulu mwenyewe lakini narudi, nilimsamehe lakini kabla ya kumsamehe hakukuwa na jambo la kusamehe

Wakati wa Jacque Maribe sikuwa katika maisha ya Jowie na sasa ambapo nipo katika maisha yake hayupo, kitu ambacho naweza sema kitu chema huwa kinafichwa." Musangi Alizungumza.

Musangi alisema kuwa Jacque hajawahi kuwa tishio kwake naye hajawahi kuwa tishio kwa Jacque.