Uhuru: Watu 5 wafariki huku 213 wakipatikana na covid 19

Uhuru
Uhuru
Rais Uhurukenyatta ametangaza kwamba visa vya covid 19 vimepungua nchini huku akisema watu 213 ndio waliopatikana na ugonjwa huo katika saa 24 zilizopita .idadi hiyo sasa inafikisha jumla ya visa hivyo nchini kuwa 33,016.

Rais Kenyatta amesema watu 5 wameaga dunia na kufikisha idadi ya walioaga dunia hadi sasa kuwa 564. Hata hivyo kuna habari njema baada ya watu 241 kupona na kufikisha jumla ya idadi ya waliopona kuwa 19 296.

Uhuru  amesema mengi zaidi yanafaa kufanywa ili kuthibiti maambukizi ya virusi hivyo ambayo sasa yamekita kambi katika kaunti na maeneo ya mashambani . Akilihutubia taifa rais alitangaza kuundwa kwa jopo maalum la Covid kujadili hatua za kuainisha mfumo wa huduma za afya katika kaunti na serikali kuu ili kuboresha sekta ya afya .