Nilikuwa karibu nikate tamaa, nilikuwa na dalili zote za ukimwi-Bensoul

Msanii Benson Mutua almaarufu Bensoul amezungumzia na kuweka wazi kuhusu maisha yake ya awali, huku akizungumzia jinsi alikuwa mgonjwa hadi alikuwa akate tamaa katika tasnia ya muziki.

Pia msanii Bensoul alieleza jinsi baba yao alitoka katika familia baada ya hao kukataa kubadili dini.

"Nilizaliwa na kulelewa maeneo ya Embu, tuulishi katika maeneo duni yaani 'slums' yanayofahamika kama Dallas nimelelewa na mama pekeyake kwa maana baba alitutoka, nina dada mkubwa ambaye alinilea." Alizungumza Bensoul.

"Babangu pia alikuwa msanii alikuwa anaimba kwa choir alikuwa anacheza pia na bendi fulani lakini alijaribu kunisimamisha nisifanye mziki lakini mziki imekuwa a part of me kutoka nikiwa kama three years old

Nilikuwa mgonjwa sana nilienda kupimwa ukimwi kwa maana nilikuwa na dalili zote za ukimwi lakini nilipatikana na kifua kikuu, nilikuwa karibu kukata tamaa katika mziki wangu." Alieleza Bensoul.

Dada yake alisema kuwa ni wakati ambao uliumiza sana kuona Bensoul akiwa mgonjwa vile.