Mhubiri huyo ambaye kwa sasa alihamia mji mwingine na kufungua kanisa kutumia jina tofauti mwaka wa 2017 alidaiwa kuwapachika mimba wanawake 12 wa kanisa lake na kati yao 7 walikuwa ni wanawake katika ndoa zao . Maandamano makubwa yalizuka wakati tabia yake ilipogunduliwa na watu wa kanisa hilo na kwa pamoja jumapili moja walilivamia kanisa hilo na kulibomoa huku mhubiri akiponea kwa kutoroka kupitia mlango wa nyuma .
Baadaye wanawake wengi ambao hawaku wameolewa walisimulia jinsi alivyowahadaa kwamba atawaoa na pindi waliposema wana mimba yake aliwapa pesa wazitoe mimba na kuruka kwa msichana wa pili kanisani ambaye pia baada ya muda alijiata katika hali kama hiyo .
Kuna wanawake ambao waliachwa na waume zao baada ya ufichuzi huo kutolewa kuhusu walivyokuwa wakilala na mhubiri .Wale waliojifungua watoto ,ambao walidaiwa kuwa wa mhubiri huyo waliachwa na waume zao na hadi leo hajawahi kuajibikia vitendo vyake .Jaribio la baadhi ya wanawake hao kutaka mahakama iwasaidie ili jamaa atoe pesa za kuwalea wanao zimegonga mwamba .
Katika mji alikohamia ,jamaa alijenga kanisa jipya huku wenyeji wasijue mbona alikwepa Ongata Rongai na huenda pia makubwa yake yakamfuata katika kanisa lake jipya .