'Vivian tafadhali heshimu kazi za watu wengine,'Msanii Vivian apokea kejeli baada y kusema haya

Msanii Vivian alishambuliwa na baadhi ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii hii ni baada ya kudai kuwa malkia wa mitandao ya tiktok Azziad Nasenya alikataa kuucheza wimbo wake na Stivo Simple Boy bure.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii, video yake akizungumza na kuelezea mwanahabari mmoja wa humu nchini kuhusu jambo hilo.

"Kuna influencer sahi at the moment anavuma sana pale tik tok na tulimuongelesha tukamuuliza kama anaweza share song yangu an Stivo akasema tumlipe.” Alizungumza Vivian.

https://twitter.com/ItsMoran_/status/1299061853008605184

Usemi wake msanii huyo haukuenda vyema bali alikejeliwa na mashabiki na wakenya wengi huku wengi wakiomba aweze kupa kazi za wenyewe heshima kwa maana pia nao wanaheshimu kazi yake.

Hizi hapa baadhi ya hisia za wakenya wengi.

kikiTheReporter: we don't dance for leisure right...lazima tulipwe ...vivian plz respect other people hustle we respect yours....

Ongaiboi:I have been a fan of Vivian and I don't watch her videos for free, bundles and phone/TV need money. So why not pay Azziad. Acheni vijana waomokeeeee!!!!!! Vijanaaa tuomokeeee nasema vijaaaanaaa tuomokeeee

MonroseMurugi: The entitlement some celeb "gatekeepers" have is astounding. Vivian expected Azziad to promote her song with Stivo Simple Boy for FREE. Producer, cameramen & director were paid lakini marketing & dancing ikuwe free? Why? It's #Azziad's job