Gavana wa Nairobi Mike Sonko attoa sehemu ya gharama ya mazishi ya Kevin Oliech ambaye aliaga dunia mwezi ulioppita .
Kevin ni kakake mchezaji wa zamani wa Harambee Stars Denis Oliech na aliaga dunia kutokana na kansa katika hospitali moja mjini Berlin ,Ujerumani agosti tarehe 16 mwaka huu .
Kupitia twitter , Sonko amesema atalipia baadhi ya gharama za mazishi ya Kevin . amesema alimjua marehemu kupitia kakake Denis huku akimsifia kama mwanasoka stadi ka tu kaake Denis .
Kevin alizichezea timu za Nairobi City Stars kisha baadaye Mathare United .Mwili wake utawasili katika uwanja wa ndege wa JKIA siku ya alhamisi .
Utahifadhiwa katika Umash Funeral Home kisha usafirishewe siku ya ijumaa kwa mazishi Seme siku ya jumamosi .