'Endeleeni kumuunga baba na Uhuru Kenyatta mkono,' Sonko awaambia wananchi wa Kisumu

Hku akihudhuria mazishi ya mwendazake mwanakandanda Kevin Oliech ambaye alikuwa nduguye kiranja ya timu ya Harambee Stars Dennis Oliech ambaye aliaga dunia akiwa ujerumani akipokea matibabu ya saratani, hii leo Sonko aliwashukuru wakazi wa Kisumu kwa kumkaribisha na heshima kubwa.

Huku walinzi wake wakijaribu kutafuta njia katika ukumbi wa vijana wa eneo hilo, nguvu zao zilifua dafu baada ya vijana hao kusema gavana Mike Sonko awahotubia mwanzo ili aweze kuhudhuria mkutano wa mazishi ya mchezaji huo.

Hakuwa na jambo la kufanya alifungua gari lake na kuwahotubia vijana hao, alipokuwa anazungumza aliwashauri wenyeji waweze kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta na Raila kwa umoja wa taifa.

"Watu wa Kisumu nina furaha kwa maana mmenikaribisha vyema humu, nataka kuwashauri na kuwaambia mwendelee kumuunga baba na rais Uhuru Kenyatta mkono

Kwa ajili ya umoja wa taifa letu." Alisema Sonko.

Pia alizungumzia kutokuwa na kazi kwa vijana huku akisema handisheki ijayo itashughulikia shida hiyo.

"Najua vijana wengi huku kisumu hawana kazi, nawahakikishia kuwa serikali na hendisheki ijayo itashughulikia jambo hilo."