Acheni kujipiga kifua! Ruto ajibu makombora ya mawaziri wanaomdunisha

Naibu rais William Ruto siku ya Jumapili aliwajibu baadhi ya mawaziri katika serikali ambao wamekuwa wakidunisha wadhifa wake.

Naibu rais ambaye alikiwa akihutubia wananchi katika eneo la Athi River, Kaunti ya Machakos aliwatahadharisha maafisa wa serikali dhidi ya Kujipiga kifua badala ya kuwatumikia wananchi.

Katika usemi ambao ulionekana kuwalenga rais Uhuru Kenyatta na kinara wa upinzani Raila Odinga Ruto alisema kwamba kuna baadhi ya watu wasiotaka kuona mtu kutoka familia maskini akitawala Kenya.

Soma habari zaidi hapa;

"Kuna wale wanasema eti hurstler hawezi kuwa rais wa Kenya, lazima baba yako awe amejulikana," Ruto alisema.

Naibu rais alikuwa akijibu matamshi ya waziri wa mazingira Kerioko Tobiko aliyemtaka yeye na wandani wake kumheshimu rais ikiwa pia yeye (Ruto) anataka kuheshimiwa.

Soma habari zaidi hapa;

Tobiko aliyekuwa ameghadhabishwa na matamashi ya seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen alisema kwamba Ruto ni karani tu wa rais kama mawaziri wengine.

“Huyu mkubwa wake ni karani ya rais…na vile mimi namheshimu rais hata huyo deputy na huyo Murkomen wamheshimu rais,” Tobiko alisema.

Akijibu matamshi hayo, Ruto akiwa Athi River baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili aliwataka mawaziri hata wale wanaotaka kujiunga na siasa kuacha kiburi na kungoja wakati kampeini zitakapoanza ili wao pia wajitose uwanjani.

"Wakenya wana akili wanajua nani tapeli," naibu rais alisema.