Raila akejeli maseneta wanaokataa pesa katika mfumo mpya wa ugavi wa mapato

Kinara wa upimzani Raila Odinga ameonekana kuunga mkono mfumo mpya wa ugavi wa mapato unao pendekezwa na kamati ya bajeti ya seneti.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kaunti ya Kakamega Raila alionekana kumkejeli seneta wa kaunti hiyo Cleophas Malala kwa kukataa kuunga mkono mfumo uliyokuwa unaipa kaunti yake mgao zaidi wa pesa.

Soma habari zaidi hapa;

"Ukiona kama kuna seneta, watu wake wanapata pesa anakataa sio eti yeye anapenda wale wengine zaidi kuna nuksi, kuna swali, ujiulize..na hiyo jibu inatoka kwa wao sio mimi," Raila alisema

Kiongozi huyo wa ODM alisema kwamba kazi ya seneta ni kuleta rasmali kwa kaunti zao na sio kuzikataa.

Raila hata hivyo alielezea imani yake kuwa seneti itaweza kupata suluhisho kwa suala hilo ambalo limepelekea seneti kuahirisha vikao vyake kwa mara tisa.

Soma habari zaidi hapa;

Seneta wa Kakamega Cleophas Malala ni miongoni mwa maseneta ambao waliungana na wenzao wa kaunti ambazo zitapoteza mabilioni ya pesa ikiwa mfumo unaoungwa mkono na serikali utapitishwa.

Baadhi ya wabunge kutoka eneo la Pwani walimkosoa Raila kwa kuonekana kuunga mkono mfumo huo ambao unazipokonya kaunti za Pwani mamilioni ya pesa.