'Wakenya wana umoja kuliko viongozi,'Mike Sonko Adai

Baada ya habari yao kuenea sana kwenye mitandao ya kijamii wakizozania penseli hatimaye walipata mahali pazuri pakulala, hii ni baada ya wakenya kuungana na kuwajengea jumba la kupigiwa mfano.

Video ya watoto hao wakizozania penseli ilitamba sana kwenye mitandao ya kijamii na hata kumfanya naibu rais kukutana nao nyumbani kwake Karen.

Huku gavana wa Nairobi Mike Sonko akizungumzia kitendo hicho cha kuwajengea nyumba kwenye mitandao yake ya kijamii alidai kuwa wakenya wana umoja kuliko viongozi wenyewe.

Huu hapa ujumbe wake;

"Baraka za Mungu hujificha, jambo moja ambalo nakubali ni kuwa wakenya wana umoja kuliko viongozi wetu, na mahali kenya imefika naona wakenya watashikana na wataamua jinsi hii nchi itaenda mbele." Aliandika Sonko.

https://twitter.com/MikeSonko/status/1302935061835264003

Pia aliwapongeza wakenya ambao walifanya kitendo hicho cha ukarimu na moyo mwema licha ya janga la corona ambpo wengi walipoteza kazi zao na hata biashara nyingi kufilisika.

"Nawashukuru wakenya wote na mashirika ambao walichangia kwa kitendo hiki kizuri kusaidia familia hii ya Nyandarua, licha ya changamoto na hali ya uchumi ilivyo kufuatia janga la corona

Haba na haba hujaza kibaba."