'Wengi wanasema kuna siri kati yangu na Uhuru ya kumtapeli Raila,'Ruto ajibu

Je kuna siri kati ya rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto ya kumtapeli kinara wa NASA Raila Odinga? haya hapa majibu ya swali lenu ambalo naibu wake Uhuru aliweza kujibu akiwa kwnye mahojiano.

Huku akiwa kwenye mahojiano Ruto alikana kuwepo na siri kati yake na Rais Uhuru Kenyatta ya kumtapeli Raila Odinga kupitia hendisheki.

"Kuna watu ambao huwa wanasema kuwa kuna siri kati yangu na rais kwanini tufanye hayo kama viongozi? Mungu ametupa uongozi na hatuwezi kuwa watapeli

Hiyo haitakuwa heshima kwa Mungu na wananchi wa kenya, sijawahi jihusisha kwa mambo kama hayo." Ruto Alisema.

Ruto alidai kuwa maneno hayo yalisemwa na watu wa karibu sana na rais na wala si kutoka kwa mdomo wa rais Uhuru Kenyatta.

"Watu hawa hawazungumzi wala kutoa matamshi hayo kwa niaba ya rais kwa maana na mjua vyema, si mtapeli wa siasa wala msaliti 

Hivi karibuni watu hawa wataachwa waende."