Kila kitu feki! Sikiza kuhusu mambo wanayofanya wanawake kuwavutia wanaume+Podi ya Yusuf Juma

HIP
HIP
Umekuwa ni mtindo wa kisasa kwa wanawake kubadilisha vitu vingi katika  miili yao ili kuwavutia au kurembeka lakini wanalipia kwa gharama ya juu sana  na wengine hata wanalipia kwa  maisha yao .

Kutoka kuchubua ngozi ili kuwa weupe hadi kuongezea ukubwa wa baadhi ya sehemu zao ,kuna kemikali na tembe ambazo wanawake wanazitumia kuyaafikia hayo na kuhatarisha maisha yao . Je mbona kuna shinikizo kwa wanawake kubadilisha muonekano wao?

Sasa pametokea pia mashine nyingine ya kumfanya mtu ‘kupunguza umri’ wake . Kando na tembe na krimu zinazotumiwa kurejesha ‘Ubikra’ pia kunazo dawa za kuongeza ukubwa wa makali na hata  sehemu nyingine  za mwili .

Sikiza kuhusu yote wanayofanya wanawake ili kujibadilisha kwa lengo moja tu ,kuvutia Zaidi . na hata tazama kwa makini unayezungumza naye ama kuanza mahusiano naye huenda siye unayemdhania kwani huenda amebadilisha kitu