Ruto ajitenga na matamshi ya Sudi na Johana Ng'eno waliomdhalilisha rais na familia yake

Naibu rais Willian Ruto amejitenga na matamshi ya chuki na matusi yaliyotolewa na wandani wake Mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng'eno na mwenzake wa Kapseret Oscar Sudi.

Ruto kupitia ujumbe kwa mtandao wa Twitter alionya viongozi na kuwataka kuacha kutumia matusi la lugha chafu dhidi ya wakenya wenzao.

"Viongozi wanafaa kujizuia na kujiepusha na matusi na kutumia lugha chafu dhidi ya wakenya wenzao. Maneno yasiofaa dhidi ya kinamama na kiongozi wa taifa ni hapana, hapana. Hakuna kiwango cha hasira kinachompa mtu uhuru wa kutumia lugha ya matusi. Kuna njia za heshima za kupitisha ujumbe hata kama unahisi machungu," Ruto alisema.

@WilliamsRuto

Leaders should exercise restraint and avoid insults and bad language against other kenyans.Unsavoury words against mothers and Head of State is a NO, NO. No amount of anger justifies use of offensive insulting language.There exists decent ways to communicate however one feels.

Matamshi ya naibu rais yalijiri muda mfupi baada ya video kuchipuka katika mitandao ya kijamii ya mbunge wa Kapseret Oscar Sudi akimsuta rais Uhuru Kenyatta na familia yake.

Sudi alikuwa akizungumzia kukamatwa kwa mbunge wa Emurua Dikirr Johanna Ng'eno aliyekamatwa siku ya Jumatatu alasiri kuhusiana na madai ya kutoa matamshi ya chukina kudhihaki rais Kenyatta.

Naibu rais siku ya Jumapili alitoa wito kwa viongozi nchini kuacha kujipiga kifua na badala yake kuhubiri amani.

Licha ya wandani wake kuonekana kumkosoa rais Uhuru Kenyatta na hata kumdhalilisha katika mikutano ya hadhara naibu rais hajawahi kumkaripia wala kumkosea heshima mkubwa wake hadharani.

Soma habari zaidi hapa: