EACC yavamia afisi za shirika la Kemsa kuhusu sakata ya shilingi bilioni 7.8

KEMSA 2
KEMSA 2
Maafisa kutoka tume ya EACC wamevamia afisi za shirika la kemsa jijini Nairobi .makachero  walifika katika afisi hizo mwendo wa saa tatu unusu asubuhi  na kufunga lango kuu la makao hayo huku wafanyikazi wa kemsa wakizuia kuondoka .

Kompuyta kadhaa zilioekana zikitolewa katika afisi hizo za kemsa  huku ulinzi ukiimarioshwa wakati wa oparesheni hiyo . wanacham wa Bodi ya shirika hilo walihojiwa  siku ya jumanne  katika makao makuu ya Eacc kuhusu jinsi dawa na vifaa vya kukabiliana na virusi vya corona zilivyonunuliwa baada ya kuzuka madai ya njama za wizi wa fedha kupitia utoaji wa kandarasi kwa njia isiofaa .

Wanasiasa takriban watano ,maafisa wakuu wa serikali na wakurugenzi 50 wa kampuni zilizohusishwa na sakata hiyo ya kemsa wanatarajiwa kuhojiwa na EACC .

Duru zaarifu  kwamba tume hio inawalenga wanasiaa kutoka erikalini na upinzani ambao wamehusishwa na wizi wa fedha katika shirika hilo kupitia kampuni zinazohusishwa nao