Polisi azirai na kufa baada ya kumpiga kofi jamaa mmoja Kakamega

Afisa mmoja wa polisi amezira na kisga kuaga dunia siku ya jumatano  baada ya kumzaba jamaa mmoja kofi aliyekuwa amejumuika nawe kula miraa katika kaunti ya kakamega

Polisi huyo  Remko Madowo  alikuwa ameketi katika eneo la  kula Miraa kwenye kituo cha kibiashara cha Malava wakati mwanamme mmoja ambaye hakutambuliwa alipojiunga naye .

Kulingana na ripoti ya polisi katika kituo cha Kabras  Madowo alimuuliza jamaa huyo mbona alikuwa ameketi hapo naye na kumzaba makofi mawili . Bila kusema jambo mwanamme huyo aliamka na kuondoka huku akiapa kuripoti tukio hilo katika kituo cha polisi .

Polisi huyo wakati huo huo alianguka  na alipokimbizwa hospitalini ,madaktari walisema alikuwa ameaga dunia .

Madowo alikuwa  amehamishwa kutoka kituo cha polisi cha Kabrqas  hadi katika kituo cha Kongit huko Bungoma .Alikuwa amerejea Kabras kuchukua vitu vyake