Je, Kuna tatizo mwanamke akimzidi mume umri?+Podi ya Yusuf Juma

Kwa muda mrefu imekuwa mtindo ama jambo la kawaida kwa wanaume kujihusisha na mahusiano na wasichana wa umri mdogo au mtu anapooa  mkewe huwa ni mtu umri wa chini kumliko .

Lakini mambo ya  usasa na  wanawake kujiamini na kujua haki zao ,basi uwanja umeswazishwa na sasa kuna mahusiano na hata ndoa ambazo mwanamke ndiye aliye na umri wa juu kumliko mumewe .

 Kumekuwa na mjadla kuhusu umri katika mapenzi na iwapo mapenzi yanayohusisha mwanamke mwenye umri wa juu kumliko mwanamme hufaulu . Kulingana na utafiti wa kijamii ,umri hauna athari yotote kwa mapenzi ili mradi wanaopendana wafahamu kwamba mapenzi yao hayategemei tofauti ya umri wao .

Katika Podi hii tunakupa mifano na jinsi uhusiano kama huo unavyoweza kudumishwa bila kutilia mkazo suala la umri au mwanamke kumzidi umri mumewe